Bado tupo nyuma utekelezaji mikataba ya haki na usawa wa kijinsia.

tngp
Mwanasheria na mtaalamu wa masuala ya Jinsia. Hussein Sengu akiwezesha juu ya Mikataba ya haki za kijinsia ya kikanda na kimataifa ambayo imesainiwa lakini bado haijatungiwa sheria (domestication) mpaka sasa

Azimio la kuwepo kwa MKATABA (itifaki) ya Jinsia na Maendeleo kwa nchi za SADC limekuwa ni chachu ya maendeleo na jinsia kwa nchi nyingi za ukanda wa kusini. Iikiwa na vigezo vipatavyo 30 vya kufikia malengo yaliyoainishwa ilI kuweza kuwa na usawa wa kijinsia Unaolenga maendeleo kwa nchi wanachama, hatua hii ya mafanikio ni ya kwanza katika dunia na imeiweka jumuiya ya SADC katika Continue reading Bado tupo nyuma utekelezaji mikataba ya haki na usawa wa kijinsia.

Jane Magigita. na Mwanamke Sokoni..!

magigita
Jane Magigita.  Mkurugenzi mtendaji wa EFG. na mshindi wa Tuzo ya Martin Luther king.

Huwezi kuzungumzia harakati za kumkomboa mwanamke mjasiriamali na wa hali ya chini hapa Tanzania bila kutaja Jina ‘Jane Magigita’. kama wewe unamsikia juu kwa juu soma kwa makini habari fupi hii.

Kwa mujibu wa takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa hali ya kiuchumi duniani katika sekta ya wafanyabiashara wadogo inaendelea kukua hivyo kutoa changamoto kubwa katika kuhakikisha inawekewa mazingira mazuri ya kisera na kisheria .
Wafanyabishara wadogo ni wengi sana hivyo wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa kutokana na uwepo wa asilimia zaidi ya 43% ya wajasiriamali wanawake Tanzania.

Ukizungumzia tu Mfanyabiashara mdogo bila kuweka makundi, umuhimu kwa jamii, na takwimu kijinsia utashindwa kupanga mipango ya maendeleo lakini pia utashindwa kujua mchango wa kila kundi katika shughuli za maendeleo katika jamii fulani au taifa kwa ujumla.  chukua tu….  Continue reading Jane Magigita. na Mwanamke Sokoni..!

JINSIA NA MAENDELEO / GENDER AND DEVELOPMENT