Jane Magigita. na Mwanamke Sokoni..!

magigita
Jane Magigita.  Mkurugenzi mtendaji wa EFG. na mshindi wa Tuzo ya Martin Luther king.

Huwezi kuzungumzia harakati za kumkomboa mwanamke mjasiriamali na wa hali ya chini hapa Tanzania bila kutaja Jina ‘Jane Magigita’. kama wewe unamsikia juu kwa juu soma kwa makini habari fupi hii.

Kwa mujibu wa takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa hali ya kiuchumi duniani katika sekta ya wafanyabiashara wadogo inaendelea kukua hivyo kutoa changamoto kubwa katika kuhakikisha inawekewa mazingira mazuri ya kisera na kisheria .
Wafanyabishara wadogo ni wengi sana hivyo wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa kutokana na uwepo wa asilimia zaidi ya 43% ya wajasiriamali wanawake Tanzania.

Ukizungumzia tu Mfanyabiashara mdogo bila kuweka makundi, umuhimu kwa jamii, na takwimu kijinsia utashindwa kupanga mipango ya maendeleo lakini pia utashindwa kujua mchango wa kila kundi katika shughuli za maendeleo katika jamii fulani au taifa kwa ujumla.  chukua tu…. ..mfano wa wafanyabiashara wa masokoni, ambao ndio wanatupatia chakula cha kila siku, wanahakikisha kuwa mkulima anaandaa chakula bora na safi wao wanakileta karibu na wewe hapo sokoni. soko limekuwa ni sehemu muhimu sana si tu katika kutuletea walaji chakula karibu bali katika kukuza kipate cha serikali zetu za mitaa (halmashauri) kupitia ushuru. unaweza usiamini ukisikia kuwa masoko katika manispaa zetu yanaingiza mabilioni…! lakini pia masoko yamekuwa ni chachu ya maendeleo ya miji yetu. na humo masokoni asilimoa kubwa ya wafanyabiashara wake ni wanawake.

Jane Magigita ni mkurugenzi mtengaji wa EFG (Equality for Growth) shirika ambalo limewalenga wanawake hawa wa masokoni kwa kutambua umuhimu wao. ameifanya kazi hiyo kwa kuwajengea uwezo, kupambana ili sera na sheria ziwe rafiki, kupelekea mpaka mazingira yao ya kazi kuwa rafiki na kuonekana ni ofisi ya heshima kajma ofisi zingine. na mwanamkee akafanya biashara kwa tija na kujikomboa.

jitihada hizo mpaka nje ya mipaka zimeonekana na akashinda tuzo kubwa sana inayotolewa na Serikali ya Marekani. wadau tuwe wabunifu katika kumomboa mwanamke. tusiishie tu kupiga kelele kwenye Ma TV na kuuza sura. safari ya mkomboa mwanamke ni mpango mikakati na utekelezaji.

namalizia na slogan ya Jane……..

“sauti ya mwanamke sokoni……..isikike”

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s