Bado tupo nyuma utekelezaji mikataba ya haki na usawa wa kijinsia.

tngp
Mwanasheria na mtaalamu wa masuala ya Jinsia. Hussein Sengu akiwezesha juu ya Mikataba ya haki za kijinsia ya kikanda na kimataifa ambayo imesainiwa lakini bado haijatungiwa sheria (domestication) mpaka sasa

Azimio la kuwepo kwa MKATABA (itifaki) ya Jinsia na Maendeleo kwa nchi za SADC limekuwa ni chachu ya maendeleo na jinsia kwa nchi nyingi za ukanda wa kusini. Iikiwa na vigezo vipatavyo 30 vya kufikia malengo yaliyoainishwa ilI kuweza kuwa na usawa wa kijinsia Unaolenga maendeleo kwa nchi wanachama, hatua hii ya mafanikio ni ya kwanza katika dunia na imeiweka jumuiya ya SADC katika mhimili wa juu katika utambuzi wa mikakati katika kushawishi utandawazi katika bara zima la Afrika na dunia kwa kuonyesha jitihada kwa upande wa kusini mwa Afrika.

Mbegu ya kwanza kabisa kupandwa Kabla ya mwaka 2008 ni Tamko (Declaration). kulikuwepo na Tamko la SADC la Jinsia na Maendeleo, ambapo nchi wanachama wakaona ni vema basi kuwepo na mkataba na kuyafanya mapendekezo yake kuwa na nguvu katika utekelezaji kuliko ilivyokuwa katika Tamko.

Mwaka 2008 Tamko likapata Baraka rasmi toka nchi wanachama na kuwa Mkataba (Protocol) ambapo nchi wanachama wakatakiwa kufanya utekelezaji wa mapendekezo yote ambayo yataishia 2015, hivo basi kuwataka Nchi wanachama kuhakikisha kuwa mapendekezo yote 30 yanatekelezwa.

Mwaka 2008 Tamko likapata Baraka rasmi toka nchi wanachama na kuwa Mkataba (Protocol) ambapo nchi wanachama wakatakiwa kufanya utekelezaji wa mapendekezo yote ambayo yataishia 2015, hivo basi kuwataka Nchi wanachama kuhakikisha kuwa mapendekezo yote 30 yanatekelezwa.

Baada ya kumaliza Kipindi walichojiwekea cha Kwanza (2008 – 2015), Nchi wanachama zilijiangaliza utekelezaji wake na kubainisha changamoto mbalimbali ambazo zilisababisha katika baadhi ya maeneo utekelezaji ukawa hafifu, changamoto hizo ni pamoja na.

Muda waliojiwekea uliorandana na Malengo ya milenia (MDGs) haukutosha Nchi mbili wanachama wa SADC hawakujiunga na wenzao 2008 – 2015 (Botswana na Mauritanias)
Mkataba (Protocol) ulikuwa na malengo lakini haukuwa na viashiria. (logical frame work was not clear). Nchi zingine zilikuwa mbel zaidi na zingine nyuma zaidi katika utekelezaji, na kuganya gepu la utekelezaji kuonaka kubwa sana Malengo mengi yalionekana kutokekelezeka kutokana msimamo wa katiba za nchi wanachama. (kukuwa). Kutokana na kuisha kwa kipindi ambach walijiwekea nchi wanachama (2008 – 2015) hakukuwa na budi ila nchi wanachama walijitathmini na kuona umuhimu wa kubosha zile changamoto na kusonga mbele, hivo basi mwaka 2015 Mkataba (Protocol) ilifanyiwa Rejea (Review) ambapo nchi wanachama walipendekeza utekelezaji mpya katika kipindi cha 2016 – 2030 na kukiita SDG tofauti na awali MDGs Mwaka 2015 nchi wanachama waliufanyia rejea (Review) Mkataba = Protocol, na kuhususha moja kwa moja mabadiliko yalenge watu, dunia, ustawi, amani, na ushirikiano. (5 Ps)

Vipaumbele kuboreshwa (likiwemo suala la katiba za nchi wanachama)kuongoza mabadiliko, na masuala ya Hali ya hewa Viashiria na utekelezaji malengo kisayansi (Logical framework) kuongoza utekelezaji Ubatizaji wa kipindi, kutoka MDGs na kuwa SDGs Kuongeza zaidi wigo wa Haki za kijinsia kwa kubadilisha maneno, vifungu, tasisi ambapo awali ilionekana kuminya wigo haki hizo. Kujiangaliza kasi ya utendaji kati ya nchi wanachama ili gepu kubwa lisijitokeze tena.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s